Friday, March 25, 2011

R.I.P KAKA VINCENT MGAZA BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA.

TANGAZO LA MSIBA
FAMILIA YA MGAZA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAO MPENDWA VINCENT GABRIEL MGAZA, KILICHOTOKEA  JANA ASUBUHI MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA KESHO HANDENI-TANGA BAADA YA MWILI WA MAREHEMU KUWASILI UKITOKEA MOSHI.
HABARI ZIWAFIKIE NDUGU WOTE POPOTE WALIPO,MARAFIKI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WOTE WA POSTA MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM,SIO RAHISI KUAMINI KUWA KAKA MGAZA HATUNAE TENA LAKINI INABIDI TUKUBALI MATOKEO,WENGI HATUTAKUSAHAU KWA UCHESHI WAKO,UKARIMU NA UTANI WAKO MUNGU AKUPUMZISHE KWA AMANI,MUME WANGU,BABA YETU,KAKA YETU,SHEMEJI YETU,MKWE WETU,MWANANGU,MJOMBA WETU HAKIKA PENGO ULILOACHA KAMWE HALIWEZI KUZIBIKA.
KAPUMZIKE KWA AMANI BABA YETU,
WANAO SARAH,MICHAEL NA BEN SISI TULIKUPENDA LAKINI BWANA KAKUPENDA ZAIDI. 

2 comments:

Anonymous said...

Tunampa pole nyingi 'Bibi Regina'na azidi kumuomba Mungu ampe moyo wa uvumilivu na ujasiri katika kuanza maisha mapya ya ujane. Kweli ni vigumu kwake kuamini lakini yote ni mipango ya Mungu kwani yeye ndie aliyemtoa Kaka Vincent na ameamua kumchukua. Jina la Bwana lihimidiwe.

Bibi Glory - TANESCO

PASSION4FASHION.TZ said...

Kwakweli ni vigumu sana kuamini,lakini hatuna jinsi inabidi tukubaliane na mapenzi ya mungu,Regina anatia huruma sana kweli itamchukua muda sana kuyazowea maisha ya ujane,kwasasa anazani bado yuko safarini atarudi tu nyumbani,kumbe maskini ndio bye bye kwa mpendwa wake,mungu azidi kumtia nguvu.

Bibi Glory haya za siku nyingi mpenzi?jamani mgao wa umeme mpaka lini? bibi Glory!!!!!karibu sana mpenzi.xx