Wednesday, April 22, 2009


3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kama ni lazima tuwalinganishe (kwani kupendeza nako ni dhana tata ajabu!) basi jibu liko wazi - ni Mama Kikwete! Kwangu mimi huyu ni wa pili kwa Mama Maria Nyerere. Ni mwakilishi halisi wa Tanzania na kila anakoenda uso wake unang'ara kwa matumaini na furaha. Japo mumewe anakabiliwa na changamoto nyingi sana (mafisadi, DECI, uchaguzi mwakani, Maisha bora kwa kila Mtanzania n.k.) lakini waweza kuyaona matumaini ya Watanzania kupitia macho ya first lady wetu. Ni lazima tusonge mbele.

PASSION4FASHION.TZ said...

Hapo umesema,hata mimi nakubaliana na wewe,na kikubwa zaidi kinachonivutia kwa huyu mama yeye ni utanzania wake kwa kwenda mbele!! mavazi yake ni vitenge na anawatumia watanzania wazalendo kumshonea nguo zake safi sanaa!!!hapo nampongeza sana kwa hilo.

Ila kama ulivyosema mume wake kaja kipindi kibaya,uchumi wa dunia umetikisika na mafisadi yamekomba kila kitu, anapambana na matatizo makubwa,hata hiyo DECI kwa upande mwingine huwezi kuilamu ni watanzania kukosa imani ya viongozi wao badala ya kuwasaidia kujikwamua kiuchumi wao ndio wamekomba mapesa yote, mabank nayo yamekuwa na masharti magumu sana kwa mtu ambae hana kitu sio rahisi kupata mikopo yao na hata wanaopata hiyo mikopo riba ni kubwa sana,sasa badala ya kumsaidia ndio wanamuongezea mzigo wa madeni.

Kwa maisha bora kwa kila mtanzania mimi kwa upande wangu bado naona nikama ndoto za alinacha.

Anonymous said...

Mimi nampa 100% mama Kikwete bwana na mavazi yake ya Kitanzania,unatuwakilisha mama yetu we love you mama.